Tuesday, June 18, 2013

RASIMU YA KATIBA MPYA INAMZUNGUMZIAJE MTOTO WA KITANZANIA.

Haki ya
mtoto
42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-
(a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,
ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika
ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya
nchi,
bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii
anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha
utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa
kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mto

Uraia wa kuzaliwa.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya
Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,
atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi
wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa
kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.

uraia wa kuandikiswa.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2),
ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo
au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE 2013)

BOFYA HAPA........

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE 2012)

BOFYA HAPA.........

Sunday, June 16, 2013

SIKU YA MTOTO WA AFRICA.



KUTOKANA NA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA,WATOTO WAISHIO VIJIJINI WAOMBA KUPATA FURSA SAWA NA WAMJINI. ZAIDI KUPATIWA ELIMU NA KUTHAMINIWA KWA KUPATIWA HAKI ZAO ZA MSINGI.