Tuesday, October 22, 2013
WATOTO WAKOSA ELIMU NA MAISHA BORA KWA UMASKINI.
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida.
Mama Sophia Lipeleta mkazi wa Nachingwea Mtwara akiwa na watoto wake walemavu pichani na kueleza kuwa alikuwa na watoto saba wa aina hiyo sasa wamebaki hawa watatu baada ya wengine kufa.
Pichani ni watoto wadogo ambao vichwa vyao ni vidogo kupindukia kwa
mujibu wa mdau Mpoki Bukuku aliyenishushia habari hii hivi punde.
Wadau kwa niaba ya mdau Mpoki Bukuku aliyeniletea habari hiii hivi punde ni kwamba
kuna watoto wa ajabu wamezaliwa kama muonavyo pichani ambao ni wa Bi Sophia Lipeleta mkazi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi ambaye alifika ofisi za gazeti la mwananchi hivi punde kwa nia ya kuomba msaada kwa wasamaria wema kwani watoto wake hawa hawawezi kuongea japokua wana umri mkubwa na kuomba kama kuna mtu atapenda kufanya utafiti anaweza kuwafanyia na kujua tatizo, lakini wako Dar na hawana chakula wala pa kulala kwani hivi sasa wanalala stendi za mabasi. Mama yao anaomba msaada wa hali na mali,nami nimeona niungane na ndugu yangu Mpoki Bukuku kuomba msaada kwa wasamaria wema ili tuwasaidie watoto hawa.
CHANZO- MZEE WA MSHITU
JE! TUNAWAANDAA WATOTO KIMAISHA?
Mtoto huyu alionekana na mpigapicha wetu katika mtaa wa mamajohn mkoa wa mbeya mjini akiwa amechoka mpaka kupelekea kulala, Baada ya kuulizwa alidai kuwa anasoma lakini akirudi shule huwa anazunguka majalalani kuokota vitu vya kuchezea,Pia wakati wa mahojiano alidai kuwa ananjaa iliyompelekea kulala katika uzio wa nyumba.
Katika mikoa mingi nchini tanzania ikiwa pamoja na mbeya ina upungufu wa viwanja vya michezo ya watoto,inayopelekea watoto kuzururazurura mtahani bila kujua wanaenda wapi.kwa hali hii tunamtengenezea mtoto mazingira mabaya ya maisha yake ya badae.
Katika mikoa mingi nchini tanzania ikiwa pamoja na mbeya ina upungufu wa viwanja vya michezo ya watoto,inayopelekea watoto kuzururazurura mtahani bila kujua wanaenda wapi.kwa hali hii tunamtengenezea mtoto mazingira mabaya ya maisha yake ya badae.
Monday, October 21, 2013
MTOTO ALIPUKIWA NA BOMU NA KUNUSURIKA KUFA NGARA.
Mtoto mmoja mkazi wa kijiji cha mumiramira kata ya bugaruma wilaya ya ngara mkoani kagera amenusurika kifo na baada ya kulipukiwa na bomu.
Hospital ya misheni rulenge wilayani humu kwa ajili ya matibabu.Mganga wa zamu wa hospital ya rulenge BI! Hilda kagaruki amemtaja mtoto huyo ni wema kigenda (12) ambaye alijeruhiwa na bomu hilo lililomkata miguu miwili na kumtoboa tumbo,Na kupelekea utumbo wa ndani kutoka nje na kupoteza damu nyingi .
Bi.kagaruki amesema majeruhi huyo alifikishwa hospitalin octoba 11/2013 majira ya saa 11 jioni.
chanzo- Bukoba wadau
Hospital ya misheni rulenge wilayani humu kwa ajili ya matibabu.Mganga wa zamu wa hospital ya rulenge BI! Hilda kagaruki amemtaja mtoto huyo ni wema kigenda (12) ambaye alijeruhiwa na bomu hilo lililomkata miguu miwili na kumtoboa tumbo,Na kupelekea utumbo wa ndani kutoka nje na kupoteza damu nyingi .
Bi.kagaruki amesema majeruhi huyo alifikishwa hospitalin octoba 11/2013 majira ya saa 11 jioni.
chanzo- Bukoba wadau
HOUSEGIRL AMNYONGA MTOTO NA KUMTUPA KWANYE DIMBWI LA MAJI.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza nasi akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.Habari na golden blog tz.
Sunday, October 6, 2013
GRADUATION MEATU SECONDARY.
SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 03/10/2013 ILIKUA SIKU YA FURAHA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ,WANAO JIANDAA KWA MTIHANI WA TAIFA UTAKAO FANYIKA TAREHE 04/11/2013. BAADA YA MAOJIANO MAFUPI NA MWANDISHI WETU WANAFUNZI WALISEMA KUWA WAMWJIANDAA VIZURI KWA MTIHANI.
MAANDALIZI YA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA PILI YAENDA VIZURI.
MAANDALIZI YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI YAENDA VIZURI MKOA WA SIMIYU,YOTE HAYO YAMEJIONESHA KATIKA SHULE YA SEKONDARI LYUSA ILIYOPO KATIKA WILAYA YA MEATU MKOA WA SIMIYU.KWANI WANAFUNZI KWA PAMOJA WAKO KATIKA HALI NZURI YA KUFANYA MTIHANI UNAO TARAJIWA KUFANYIKA KESHO TAREHE 07/10/2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)