Mtoto huyu alionekana na mpigapicha wetu katika mtaa wa mamajohn mkoa wa mbeya mjini akiwa amechoka mpaka kupelekea kulala, Baada ya kuulizwa alidai kuwa anasoma lakini akirudi shule huwa anazunguka majalalani kuokota vitu vya kuchezea,Pia wakati wa mahojiano alidai kuwa ananjaa iliyompelekea kulala katika uzio wa nyumba.
Katika mikoa mingi nchini tanzania ikiwa pamoja na mbeya ina upungufu wa viwanja vya michezo ya watoto,inayopelekea watoto kuzururazurura mtahani bila kujua wanaenda wapi.kwa hali hii tunamtengenezea mtoto mazingira mabaya ya maisha yake ya badae.
No comments:
Post a Comment