Wednesday, November 28, 2012
TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA KUOKOA MAISHA YA MTOTO.
TANZANIA IMECHAGULIWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA KIMATAIFA WA KUOKOA MAISHA YA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUPITIA CHANJO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA DUNIANI. HABARI KUTOKA GAZETI LA HABARI LEO.
Thursday, November 22, 2012
NANI ANYONYE SASA?
Tuesday, November 13, 2012
VIFO VYA WATOTO,WAJAWAZITO VYAPUNGUA TANZANIA.
Serikali imesema idadi ya vifo vya
wajawazito na watoto nchini vimepungua wakati wa kujifungua kutoka vifo
578 sawa na asilimia 28 hadi kufikia 454 (asilimia 20) kwa mwaka.
Kaimu Mganga Mkuu, Dk. Donad Mmbando, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam.
Alisema wadau wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii walikutana ili kujadili mpango wa huduma ya Kiteknolojia kwa Mama na Mtoto kwa lengo la kuboresha huduma ya uzazi wa mpango.
“Tumeamua kutoa elimu kwa akina mama na watoto kupitia taarifa zitakazotolewa na wizara juu ya imani potofu za kishirikina na ugumba,” alisema Dk. Mmbando.
Alisema mpango huo utasaidia wananchi wa vijijini kufahamu huduma hizo mahali zinapoweza kupatikana, hususan katika vituo vya afya.
Dk. Mmbando alisema wananchi wengi wa vijijini wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya uzazi wa mpango, kwa kuwa unapunguza ongezeko la idadi watoto ndani ya familia.
Hata hivyo, alisema wamejipanga kutoa elimu ya kutosha mjini na vijijini ili wananchi waondokane na imani potofu.
habari kutoka gazeti la nipashe 13/11/2013

Monday, November 12, 2012
SHINDANO LA PICHA KALI ZA WATOTO.
LENGO LA
SHINDANO HILI NI KUWALETA WAZAZI PAMOJA NA WATOTO WAO WENYE UMRI KATI YA MIEZI
0 HADI MIEZI 18.
SHINDANO
HILI NI KWA WATOTO WA KITANZANIA TU,AMBALO LITAENDESHWA KUANZIA TAREHE 1-11-2012
HADI 30-11-2012.
PIGA PICHA
NZURI YA MWANAO KISHA TUMA HIYO PICHA KWA NJIA MOJA WAPO.
TUMA BARUA PEPE KWENDA photobebi@gmail.com AU PELEKA TSN ,SHOPRITE NA MADUKA SHIRIKI AU PELEKA OFISI ZA CHEMCOTEX
ZILIPO MIKOANI YOTE TANZANIA.
CHEMICOTEX INDUSTRIES INAKUHAIDI
ZAWADI KWA PICHA BORA YA MTOTO
VIGEZO NA
MASHARTI KUZINGATIWA.HASA KWA MATUMIZI YA PICHA
ZA WATOTO KWA AJILI YA KALENDA YA BEBI.
Saturday, November 10, 2012
MTOTO ANA HAKI YA KUCHEZA.
Sunday, November 4, 2012
JE! CHOO KINA UMUHIMU GANI KATIKA JAMII HII?
KUSHOTO PICHANI CHINI NDIPO CHOO KILIPO.
PICHA CHINI INATUONESHA MANDHARI YA NYUMBA NA CHOO,
PICHANI CHINI INATUONESHA SEHEMU CHOO KILIPO.
JINSI GANI CHOO KILIVYOKUWA SI MUHIMU KATIKA JAMII HII YA MKOA WA SIMIYU WILAYA YA MEATU.HII INAONESHA KUWA NA CHOO NI KAMA KUJIHIFADHI TU,BALI SI KWA AFYA BORA.JE! TUTAWASAIDIA VIPI JAMII YA AINA HII? KAMA PICHA INAVYOONEKANA JUU.ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA CHOO INAHITAJIKA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA JAMII KAMA HII,LAKINI SIO ELIMU PEKEE INAWEZA KUWAKOMBOA WANAJAMII HAWA TU KUTOKANA NA MARADHI MBALIMBALI YANAYOWEZA KUATHIRI AFYA ZAO, BALI UTEKELEZAJI WA SERIKALI NA ASASI ZISIZO ZA SERIKALI JUU YA SERA YA AFYA BORA KWA JAMII.
Subscribe to:
Posts (Atom)