Serikali imesema idadi ya vifo vya
wajawazito na watoto nchini vimepungua wakati wa kujifungua kutoka vifo
578 sawa na asilimia 28 hadi kufikia 454 (asilimia 20) kwa mwaka.
Kaimu Mganga Mkuu, Dk. Donad Mmbando, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam.
Alisema wadau wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii walikutana ili
kujadili mpango wa huduma ya Kiteknolojia kwa Mama na Mtoto kwa lengo la
kuboresha huduma ya uzazi wa mpango.
“Tumeamua kutoa elimu kwa akina mama na watoto kupitia taarifa
zitakazotolewa na wizara juu ya imani potofu za kishirikina na ugumba,”
alisema Dk. Mmbando.
Alisema mpango huo utasaidia wananchi wa vijijini kufahamu huduma hizo
mahali zinapoweza kupatikana, hususan katika vituo vya afya.
Dk. Mmbando alisema wananchi wengi wa vijijini wamekuwa na mtazamo
tofauti juu ya uzazi wa mpango, kwa kuwa unapunguza ongezeko la idadi
watoto ndani ya familia.
Hata hivyo, alisema wamejipanga kutoa elimu ya kutosha mjini na vijijini ili wananchi waondokane na imani potofu.
habari kutoka gazeti la nipashe 13/11/2013
No comments:
Post a Comment