WANAFUNZI 560,706 WA SHULE ZA MSINGI WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA SERIKARI.JAPO YA UFAULU WAO WATALAZIMIKA KUFANYA MTIHANI MWENGINE WA KUBAINI WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
KWA MAELEZO YA DK SHUKURU KAWAMBWA WAZILI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,WANAFUNZI WALIOFAULU NI ASILIMIA 64.74 YA WANAFUNZI 865,827 WALIOFANYA MTIHANI HUO.
AWALI IDADI YA WANAFUNZI WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI HUO NI 894,839 HIVYO IDADI YA WALIOFANYA NI ASILIMIA 96.76.WATAHINIWA 29,012 SAWA NA ASILIMIA 3.24 HAWAKUFANYA MTIHANI KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI IKIWA UTORO.
ALIFAFANUA KUWA WATAHINIWA 3,087 WALIPATA ALAMA - A,WANAFUNZI 40,683 WALIPATA ALAMA - B,WANAFUNZI 22,103 WALIPATA ALAMA - C,NA WANAFUNZI 73,264 WALIPATA ALAMA - E. KATI YA WANAFUNZI 560,706 NI WASICHANA SAWA NA ASILIMIA 50.20 NA WAVALANA 279,246 SAWA NA ASILIMIA 49.80.
KUTOKANA NA TAKWIMU ZA UFAHULU WA MWAKA HUU 2012 ZINAONESHA UFAULU UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 8.8.
je hiyo idadi kubwa ya ufahulu inaendana na sifa anazotakiwa kuwa nazo mtoto anayejiunga na sekondari au tunaongeza idadi ya watoto wasiojua kusoma na kuandika katika shule za sekondari?
ReplyDelete