Saturday, December 22, 2012

UFAULU WA DARASA LA SABA KWENDA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA SERIKARI NCHINI TANZANIA WAONGEZEKA.


WANAFUNZI 560,706 WA SHULE ZA MSINGI WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA SERIKARI.JAPO YA UFAULU WAO WATALAZIMIKA KUFANYA MTIHANI MWENGINE WA KUBAINI WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
KWA MAELEZO YA DK SHUKURU KAWAMBWA WAZILI WA ELIMU  NA MAFUNZO YA UFUNDI,WANAFUNZI WALIOFAULU NI ASILIMIA 64.74 YA WANAFUNZI 865,827 WALIOFANYA MTIHANI HUO.
AWALI IDADI YA WANAFUNZI WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI HUO NI 894,839 HIVYO IDADI YA WALIOFANYA NI ASILIMIA 96.76.WATAHINIWA 29,012 SAWA NA ASILIMIA 3.24 HAWAKUFANYA MTIHANI KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI IKIWA UTORO.
ALIFAFANUA KUWA WATAHINIWA 3,087 WALIPATA ALAMA - A,WANAFUNZI  40,683 WALIPATA ALAMA - B,WANAFUNZI 22,103 WALIPATA ALAMA - C,NA WANAFUNZI 73,264 WALIPATA ALAMA - E. KATI YA WANAFUNZI 560,706 NI WASICHANA SAWA NA ASILIMIA 50.20 NA WAVALANA 279,246 SAWA NA ASILIMIA 49.80.
KUTOKANA NA TAKWIMU ZA UFAHULU WA MWAKA HUU 2012 ZINAONESHA UFAULU UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 8.8.

Sunday, December 16, 2012

JE! MAENDELEO BILA YA MWALIMU INAWEZEKANA.

NYUMBA YA MWALIMU WETU WA KITANZANIA ILIYOPO MKOA WA SIMIYU WILAYA YA MEATU KATIKA SHULE YA MSINGI NKOMA.

SABABUKUBWA INAYOFANYA TANZANIA KUWA NA UPUNGUFU WA WALIMU NI PAMOJA NA KUTOTHAMINIWA KWA WALIMU,PICHANI JUU NI NYUMBA YA MWALIMU ILIYOPO KATIKA SHULE YA MSINGI NKOMA ILIYOPO KATA YA NKOMA MKOA WA SIMIYU.SAMBAMBA NA HILI LA NYUMBA IKIWA PAMOJA NA MIUNDOMBINU MIBOVU ZAIDI KATIKA SHULE ZILIZOKO VIJIJINI.KWA STAHILI HII TUSITEGEMEE MWALIMU ATUFUNDISHIE MTOTO KWA MOYO MMOJA.JE! MAENDELEO BILA YA MWALIMU INAWEZEKANA?

Wednesday, November 28, 2012

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA KUOKOA MAISHA YA MTOTO.

TANZANIA IMECHAGULIWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA KIMATAIFA WA KUOKOA MAISHA YA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUPITIA CHANJO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA DUNIANI. HABARI KUTOKA GAZETI LA  HABARI LEO.

Thursday, November 22, 2012

NANI ANYONYE SASA?

KAMA WATOTO WANAKUNYWA MAZIWA YA KOPO AU YA VIWANDANI NANI ANANYONYA MAZIWA YA MAMA SASA.TUACHANE NA DHANA POTOFU TULIZOIGA BILA KUCHUJA NA KUZICHUKUA KAMA ZILIVYO KUTOKA KWA WAZUNGU,TUKIFIKILI KWAMBA MTOTO KUNYONYA MAZIWA YA MAMA CHUCHU ZITALALA, KITU AMBACHO MADHALA YAKE MTOTO KUKUA KWA TABU NA KUKOSA AFYA NZURI.KWANI KAMA ATAKUNYWA MAZIWA YA KOPO ATAKUZWA NA KEMIKALI MWILINI KAMA KUKU WA KIZUNGU,UKIFIKILI KWAMBA MTOTO ANA AFYA NZURI KUMBE NI MWILI WA TUFE AU PULIZO AMBAPO HATA KINGA ZA MWILI HUPUNGUA.KWA HIYO MAMA ZINGATIA NA MNYONYESHE MTOTO KWA WAKATI.

Tuesday, November 13, 2012

VIFO VYA WATOTO,WAJAWAZITO VYAPUNGUA TANZANIA.

Serikali  imesema idadi ya vifo vya wajawazito na watoto nchini vimepungua wakati wa kujifungua kutoka vifo 578 sawa na asilimia 28 hadi kufikia 454 (asilimia 20) kwa mwaka.

Kaimu Mganga Mkuu, Dk. Donad Mmbando, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam.

Alisema wadau wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii walikutana ili kujadili mpango wa huduma ya Kiteknolojia kwa Mama na Mtoto kwa lengo la kuboresha huduma ya  uzazi wa mpango.

 “Tumeamua kutoa elimu kwa akina mama na watoto kupitia taarifa zitakazotolewa na wizara juu ya imani potofu za kishirikina na ugumba,” alisema Dk. Mmbando.

Alisema mpango huo utasaidia wananchi wa vijijini kufahamu huduma hizo mahali zinapoweza kupatikana, hususan katika vituo vya afya.

Dk. Mmbando alisema wananchi wengi wa vijijini wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya   uzazi wa mpango, kwa kuwa unapunguza ongezeko la idadi watoto ndani ya familia.

Hata hivyo, alisema wamejipanga kutoa elimu ya kutosha mjini na vijijini ili wananchi waondokane na imani potofu.

     habari kutoka gazeti la nipashe 13/11/2013

Monday, November 12, 2012

SHINDANO LA PICHA KALI ZA WATOTO.


CHEMICOTEX INDUSTRIES LIMITED CHINI YA UDHAMINI WA BIDHAA ZAKE BORA ZA WATOTO ”BEBI” INAPENDA KUKULETEA SHINDANO LA KWANZA LA KITAIFA “PICHA NZURI YA WATOTO”
LENGO LA SHINDANO HILI NI KUWALETA WAZAZI PAMOJA NA WATOTO WAO WENYE UMRI KATI YA MIEZI 0 HADI MIEZI 18.
SHINDANO HILI NI KWA WATOTO WA KITANZANIA TU,AMBALO LITAENDESHWA KUANZIA TAREHE 1-11-2012 HADI 30-11-2012.
PIGA PICHA NZURI YA MWANAO KISHA TUMA HIYO PICHA KWA NJIA MOJA WAPO.
          TUMA BARUA PEPE KWENDA photobebi@gmail.com AU PELEKA TSN ,SHOPRITE NA MADUKA SHIRIKI AU PELEKA OFISI ZA CHEMCOTEX ZILIPO MIKOANI YOTE TANZANIA.
CHEMICOTEX INDUSTRIES INAKUHAIDI ZAWADI KWA PICHA BORA YA MTOTO
VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.HASA KWA MATUMIZI YA PICHA  ZA WATOTO KWA AJILI YA KALENDA YA BEBI.

Saturday, November 10, 2012

MTOTO ANA HAKI YA KUCHEZA.

PICHANI  JUU WATOTO WA MKOA WA SIMIYU WAKIWA HAWANA LA KUFANYA NA NI KIPINDI CHA MICHEZO,HII NI KUTOKUA NA VIWANJA VYA WAZI VYA MICHEZO NA KUBANWA KWA WATOTO WADOGO KOTOKANA  NA KAZI MBALIMBALI ZA NYUMBANI.TAMADUNI NYINGI ZA KIAFRIKA ZINAWABANA WATOTO WA KIKE KWA KIASI KIKUBWA KWA KAZI MBALIMBALI ZA NYUMANI, HII INADHIHIRISHWA KATIKA MKOA HUU WA SIMIYU WILAYA YA MEATU KWA WATOTO WADOGO KUCHOTESHWA MAJI,KUKATA KUNI,KUCHUNGA MIFUGO NA SHUGHULI NYINGINE KAMA KUOSHA VYOMBO.HII KWA KIASI KIKUBWA INAFANYA WATOTO KAMA HAWA KUKOSA HAKI ZAO ZA MSINGI KAMA KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO.    

Sunday, November 4, 2012

JE! CHOO KINA UMUHIMU GANI KATIKA JAMII HII?

  KUSHOTO  PICHANI CHINI NDIPO CHOO KILIPO.

               

 

 PICHA CHINI INATUONESHA MANDHARI YA NYUMBA NA CHOO,



 PICHANI CHINI INATUONESHA SEHEMU CHOO KILIPO.

         JINSI GANI CHOO KILIVYOKUWA SI MUHIMU KATIKA JAMII HII YA MKOA WA SIMIYU WILAYA YA MEATU.HII INAONESHA KUWA NA CHOO NI KAMA KUJIHIFADHI TU,BALI SI KWA AFYA BORA.JE! TUTAWASAIDIA VIPI JAMII YA AINA HII?                                                                                                                                                                 KAMA PICHA INAVYOONEKANA JUU.ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA CHOO INAHITAJIKA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA JAMII KAMA HII,LAKINI SIO ELIMU PEKEE INAWEZA KUWAKOMBOA WANAJAMII HAWA TU KUTOKANA NA MARADHI MBALIMBALI YANAYOWEZA KUATHIRI AFYA ZAO, BALI UTEKELEZAJI WA SERIKALI NA ASASI ZISIZO ZA SERIKALI JUU YA SERA YA AFYA BORA KWA JAMII.

Thursday, November 1, 2012

Thursday, October 11, 2012

KUTOKANA NA WATOTO WA KIJIJI CHA NKOMA MKOA WA SIMIYU KUKOSA MICHEZO YA WATOTO NA KUTOKAA PAMOJA"SOCIALIZE", MANAMBA INTERTAINMENT CHINI YA UNCLE CHRISTOPHER MANAMBA ILIANDAA TOTO PARTY SIKU YA NANENANE (08/08/2012).DHUMUNI LIKIWA NI 
JAPOKUWA  HAWANA MATUMAINI YA KUFAULU NA HATA AKIFAULU PIA HANA MATUMAINI YA KUENDELEA KUSOMA KUTOKANA NA JAMII KWA UJUMLA KUTOKUWA NA MUAMKO WA ELIMU NA UPUNGUFU WA WALIMU.PICHANI JUU WANAONEKANA WATOTO WA SHULE YA MSINGI NKOMA ILIYOKO KATA YA NKOMA MKOA WA SIMIYU WAKIFURAHI BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI TAREHE (20/09/2012). 

MTOTO ANA HAKI YA KUCHEZA NA KUCHANGAMANA NA WENZIE

KUTOKANA NA WATOTO WA KATA YA NKOMA MKOA WA SIMIYU KUKOSA MICHEZO INAYOWAFANYA WAKAE PAMOJA(SOCIALIZE),MANAMBA INTERTAINMENT CHINI YA UNCLE CHRISTOPHER MANAMBA ILIANDA TOTO PARTY SIKU SIKU YA NANENE(08/08/2012)NDANI YA  UKUMBI WA SADO KATIKA KIJIJI CHA NKOMA.KAMA PICHA INAVYOONEKANA HAPO JUU UNCLE CHRISTOPHER MANAMBA  AKICHANGAMANA NA WATOTO KATIKA MICHEZO MBALIMBALI. 

                         MAJI NI UHAI .       

KUTOKANA NA UHABA WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA NKOMA MKOA WA SIMIYU                INAWALAZIMU WANAKIJIJI KUCHIMBA VISIMA  KAMA PICHA INAVYOONEKANA JUU,  ILI KUJIPATIA MAJI KWA MATUMIZI YA NYUMBANI  KATIKA MTO LYUSA AMBAO UTULILISHA MAJI WAKATI WA MSIMU WA MASIKA TU.JAMII NZIMA HUTUMIA MAJI AYO JAPO HUSHEA NA WANYAMA MBALMBALI KAMA MBWA HASA NYAKATI ZA USIKU.

Monday, August 27, 2012


MTOTO AKITAZAMA NJIA YA KUTOKA KIMAISHA,JE! AENDE KULIA AU KUSHOTO?


                                       MTOTO  AKIWA KATIKA POZI          
                    MTOTO AKIFURAHIA MICHEZO YA KITOTO