Tuesday, March 19, 2013

MKUTANO WA WADAU WA ELIMU WILAYA YA MEATU.

MKUU WA WILAYA YA MEATU MAMA ROSEMARY KIRIGINI.

BAADA YA WILAYA YA MEATU MKOA WA SIMIYU KUFANYA VIBAYA KATIKA MATOKEO YA MTIHANA WA DARASA LA SABA NA NA KIDATO CHA NNE,TAREHE 30/01/2013 WILAYA ILIAMUA KUFANYA KONGAMANO LA KIELIMU KUJADILI CHANGAMOTO ZILIZOPELEKEA WATOTO KUFANYA VIBAYA KATIKA MITIHANI YAO.
LIKIONGOZWA NA MHESHIMIWA PROF EMMANUEL K. BAVU AMBAYE ALIKUA MWENYEKITI WA KONGAMANO HILO PAMOJA NA KATIBU TAWALA MKOA MWAMVUA JILUMBI,AFISA ELIMU MKOA ALOYCE KAMAMBA ,MKUU WA WILAYA ROSEMARY KIRIGINI , MKURUGENZI MTENDAJI(W) ISAYA MOSES NA WADAU WENGINE WA SEKTA MBALIMBALI. WADAU WA KONGAMANO HILO WALISEMA KUWA CHANGAMOTO ZINAZOPELEKEA KUSHUKA KWA ELIMU NI PAMOJA NA MWAMKO DUNI WA ELIMU KWA BAADHI YA WAZAZI NA WALIMU KUTOTIMIZIWA MAHITAJI YAO INAYO PELEKEA KUTOKUFANYA KAZI KWA MOYO.MWISHO KABISA WALIAZIMIA KUFANYA MAREKEBISHO ILI KUONGEZA UFAULU WILAYA YA MEATU.

No comments:

Post a Comment